Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad
Masauni, ameonya watu watakaojaribu kuleta vurugu nchi
ikielekea Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani
unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari
baada ya Kikao cha ndani na Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi
la Polisi.
