Aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA Lawrence Masha ameomba kupokelewa katika chama alichokiama wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015 ambacho ni CCM,Lawrence Masha amejiunga leo na Chama Cha Mapinduzi katika vikao vunavyoendelea vya chama hicho,Masha amesema”Nimekuja hapa kuwaombeni mnipokee mwana mpotevu nimerudi,Niko imara na nitakuwa mwaminifu kwa CCM.
Na wakili msomi aliyekuwa mwanachama wa ACT Wazalendo Albert Msando amejiunga na Chama Cha Mapinduzi leo katika vikao vinavyoendelea ndani ya Chama hicho.
Lakini pia si Lawrence Masha na wakili msomi Albert Msando pekee bali na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa CHADEMA Taifa Patrobas Katambi ajiunga rasmi CCM.
