Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaungana kutaka shitaka dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini Zambia kufutiliwa mbali.

In Kimataifa

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty limeungana na mashirika mengine yanayotaka shitaka la uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini Zambia na wenzake watano kufutiliwa mbali mara moja na kusema, ni kampeni ya mateso .Hakainde Hichilema alikamatwa baada ya kukataa kuupisha njia msafara wa rais Edgar Lungu,Kitendo kinachoonekana kama utovu wa adabu kwa rais.

Hakainde pamoja na wenzie watano ambao ni wajumbe wa chama cha United Party for National Development wamekuwa wakishikiliwa kwa zaidi wiki mbili kwa kile Amnesty ilichosema ni kosa la usalama wa barabarani na sio uhaini.

Pia Amnesty imetaka kuchunguzwa kwa tuhuma za kuteswa kwa kiongozi huyo na watu waliokuwa wamejifunika nyuso.Mashtaka ya uhaini yanaonekana kama njia moja wapo ya rais ya kunyamazisha upinzani, baada ya uchaguzi uliopingwa ambao uliambatana na vurugu.

Kwa upande wake, kiongozi huyo wa upinzani amekuwa akijitetea kwamba waliruhusiwa kuupita msafara wa rais na mamlaka kwa sababu walikuwa wakienda kwenye shughuli ya kidini

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu