Masikitiko shambulizi la kigaidi London

In Kimataifa
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anasema shambulizi la kigaidi nje ya msikiti Kaskazini mwa jiji London, linasikitisha na kuchosha.
Shambulizi hilo limesababisha kifo cha mtu mmoja na zaidi ya 10 kujeruhiwa.
Waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu hospitalini.
Bi. May amesema kuwa shambulizi hilo liliwalenga Waislamu.
Kiongozi huyo wa serikali ameongoza kikao cha usalama mapema siku ya Jumatatu na kusisitiza kuwa, Uingereza haitavumilia ugaidi na mafunzo ya kijihadi.
Ni tukio lililotokea wakati huu waumini wa dini hiyo wakiendelea kuwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Polisi wamesema watu wote waliojeruhiwa na aliyepoteza maisha, wote ni Waislamu.
Dereva wa basi liliwagonga Waislamu hao, amekamatwa na Polisi wanasema wanaamini alitekeza shambulizi hilo peke yake.
Uingereza hivi karibuni imeendelea kushuhudia matukio ya kigaidi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu