Maspika wamchagua Ndugai kuwa Mwenyekiti barani Afrika.

In Kitaifa

Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb), amechaguliwa kuwa Mwenyekiti  wa Maspika na Viongozi wa Bunge katika Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika.

Uchaguzi huo umefanyika  katika Mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika uliomalizika jana Mjini Abuja.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge ni kuwa Kwa wadhifa huo, Mhe Ndugai ataongoza Maspika wenzake toka Mabunge na Mabaraza ya kutunga Sheria  63 yaliyoko katika nchi 18 za Jumuiya ya Madola kwenye Bara la Afrika.

Wadhifa huo ni wa miaka miwili kuanzia sasa hadi mwaka 2019 kutakapofanyika uchaguzi mwingine.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mabunge Barani Afrika ni pamoja na Afrika  ya Kusini, Botwana, Cameroon ,Ghana, Kenya, Lesotho,   Msumbiji, Mauritius, Malawi, Nigeria, Namibia, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Swaziland, Tanzania, Uganda na Zambia.

Akizungumzia uchaguzi huo,  Mhe Ndugai amesema anawashukuru Maspika Wenzake kwa kumpa dhamana na heshima lakini zaidi kwa Tanznaia na kwamba bunge litaendelea kung’ara.

Huu ni wadhifa wa nne kwa Mhe. Ndugai katika masuala ya Bunge kwenye medani ya Kimataifa. Amewahi kuwa Mwakilishi wa Nchi za Afrika Mashariki katika Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Duniani mwaka 2008-2011, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ya Umoja wa Mabunge ya Afrika, Pacific na Carribbean na Jumuiya ya Ulaya  mwaka 2011-2014 na Rais wa Baraza la Mabunge ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC – PF)

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu