Mataifa ya Africa Mashariki na kati yaungana na mataifa mengine kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi duniani.

In Kimataifa

Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati yameugana na mataifa mengine duniani kuadhimisha sikukuu ya Wafanyikazi duniani siku ya Jumatatu.

Haya ni maadhimisho ya kila mwaka na siku kama yatarehe moja ambapo , wafanyakazi duniani hutumia kudai nyongeza ya mshahara na kutaka kuthaminiwa na waajiri wao.

Kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, wafanyikazi wamekuwa wakishinikiza nyongeza ya mshahara kutoka kwa waajiri wao ili kumudu hali ngumu ya kiuchumi inayowakabili.

Vyama vya wafanyikazi kote duniani na hata barani Afrika mfano wa COSATU nchini Afrika Kusini na COTU nchini Kenya, vimekuwa na ushawishi wa kisiasa kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wanachama.

Nchini Kenya, maadhimisho ya mwaka huu yaliongozwa na rais Uhuru Kenyatta ambaye alitumia siku hiyo kuhimiza uchaguzi wa amani mwezi Agosti mwaka huu.

Aidha, ametangaza kuwa mshahara wa wafanyikazi nchini humo umeongezwa kwa asilimia 18, kuanzia mfanyikazi anayepata mshahara wa chini wa Dola 130 kwa mwezi.

Kiongozi huyo pia ameelezea mafaniko ya serikali yake kwa muda miaka minne iliyopita, ikiwa ni pamoja na kufufua viwanda vilivyounda nafasi zaidi za kazi.

Nchini Tanzania rais John Magufuli naye, amesema wafanyikazi nchini humo wameamua kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya kufikia uchumi wa viwanda nchini humo.

Aidha, ameeleza kuwa madai ya wafanyikazi nchini humo ikiwa ni pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii ,kuwalipa fedha zao ikiwa watapoteza kazi kabla ya kustafu, linashughulikiwa na serikali yake.

Nchini Uganda, rais Yoweri Museveni amewataka wafanyikazi nchini humo kuijenga Uganda kupitia sera nzuri.

Nchini Ugiriki maelfu ya wafanyikazi wameandamana jijini Athens na kutangaza mgomo wa siku nzima, kushinikiza serikali kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Serikali ya Ugiriki imepanga kupunguza kazi na mishahara katika sekta ya  umma tarehe 17 mwezi huu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu