Mawaziri sita waishio uhamishoni kuhukumiwa

In Kimataifa

   Kesi ya serikali iliyopita ya Blaise Compaoré  imeikilizwa tena  jana asubuhi May 4 katika Mahakama Kuu mjini Ogadugu.

Mawaziri sita wanaoishi uhamishoni watahukumiwa licha ya kutokuwepo.

Rais wa zamani, ambaye anachukuliwa kama waziri wa ulinzi wa zamani, ambaye alichukua uraia wa Co devowa atahukumiwa pia licha ya kutokuwepo.

Viongozi hao wa zamani wanashtumiwa “mauaji ya kukusudia na kula njama kwa kuwapiga na kuwajeruhi, kwa kukusudia waandamanaji.

Mbele ya mahakimu, mawaziri 25 wa zamani watasikilizwa kesi hiyo

Wote wanashtumiwa kwa kuwa waliamua katika kikao cha baraza la mawaziri cha Oktoba 29, 2014, kutoa wito kwa jeshi kukomesha waandamanaji waliokua wakipinga marekebisho ya Katiba.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, mawaziri walitoa wito wa kwa majeshi kuwafyatulia risasi waandamanaji, na kusababisha vifo vya watu saba na 88 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha mahakama, kesi haitadumu zaidi ya wiki mbili.

chama Compaore tayari kimeshutumu kwamba “kesi hiyo ni ya kisiasa”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu