Mawaziri wa nchi za Umoja wa Ulaya wamempa muongozo mpatanishi wa umoja huo anayehusika na suala la Uingereza kujitoa kutoka umoja huo Brexit, Michel Barnier.
Mwanadiplomasia huyo wa zamani wa Ufaransa hatarajiwi kuanzisha mazungumzo ya Brexit mpaka baada ya uchaguzi mkuu wa Uingereza mwezi ujao.
Mawaziri kutoka nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wameridhia kanuni ambazo mpatanishi mkuu Barnier atazitumia kujadili kujitoa kwa Uingereza.
Barnier binafsi amesema hataki kufikiria kuhusu mazungumzo hayo kuvunjika na kwamba pande zote mbili huenda zikajadili mkataba wa kibiashara ikiwa masuala muhimu yanayohusiana na Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya yatakubaliwa haraka.
