Mawaziri watano watembelea mpaka wa Tanzania na Uganda.

In Kitaifa

Mawaziri watano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wametembelea mpaka wa Tanzania na Uganda ili kutatua changamoto zinazoukabili mpaka huo na kuuboresha.

Mawaziri hao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji , Mhandisi Isack Kamwelwe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya ardhi, miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa na mawaziri hao ni eneo la mpaka ya Tanzania na Uganda kwa upande unapopita mto Kagera na eneo la kivuko cha mpaka wa Tanzania na Uganda kilichopo Mtukula mkoani Kagera.

Katika ziara hiyo, mawaziri hao walijionea hali halisi ya maisha ya wakazi wa mipakani na jinsi wanavyohusiana na wenzao wa nchi ya jirani ya Uganda, ambapo wamekuwa wakishirikiana na kuishi kwa amani katika shughuli zao za kila siku.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu