May amtaka Putin kuacha kuingilia uchaguzi wa nchi.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameishutumu vikali Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa nchi na kuendesha uhalifu wa mitandao.

Akiongea mjini London May alisema kuwa serikali ya Vladimir Putin anajaribu kuhujumu nchi zilizo huru.

Bi May alisema kuwa Urusi ilikuwa ikiunda taarifa za uongo dhidi nchi za magharibi.

Lakini akaongeza kuwa kwa sababua Uingereza haitaki makabiliano na Urusi italazimika kulinda maslahi yake.

Matamshi yake ni kinyume na yale ya rais wa Marekani Donald Trump ambaye alisema wiki iliyopita kuwa anaamini kuwa Trump hakuingilia uchaguzi wa Marekania mwaka 2016

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kuzuru Urusi mwezi ujao.

May alisema kuwa Putin ni lazima afuate mkondo mwingine kutoka kwa ule amechukua hivi karibuni ikiwemo kulimega eneo la Crimea , mzozo nchini Ukrain na mashambulizi ya mitandao kwa serikali za nchi na mabunge kote Ulaya.

Urusi inawez kuwa mshirika muhimu wa nchi za magharibi ikiwa tu itafuata sheria, alisema May.

Exit mobile version