Mazungumzo ya kupunguza umaskini barani Afrika yafunguliwa Addis Ababa

In Kimataifa

Mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu maendeleo na kupunguza umaskini barani Afrika, na Mkutano wa jopo la washauri bingwa wa China na Afrika yamefunguliwa jana katika kituo cha mkutano cha Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw Wang Yi na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw Moussa Mahamat wamehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa mkutano huo.

Bw Wang Yi ametoa hotuba akisema watu milioni 400 wa Afrika wanaishi katika umaskini, na Wachina zaidi ya milioni 40 wanahitaji kuondokana na umaskini hivyo Ni wajibu wa China kushirikiana katika kupambana na umaskini na kupata maendeleo ya pamoja, ambalo ni lengo la pamoja, na ni mahitaji ya maendeleo ya kijamii.

Amesema, “China inapenda kuzidisha mawasiliano na nchi za Afrika kuhusu uzoefu wa kutawala nchi, kutafuta njia ya maendeleo na kupunguza umaskini kwa kufuatana na mahitaji ya nchi za Afrika. China inapenda kubadilishana uzoefu na marafiki zetu za Afrika.”

Bw Moussa Faki Mahamat amesema anapenda ushirikiano wa pande mbili katika kupunguza umaskini upate mafanikio.

Katika mkutano huo, wataalamu na wasomi wa Afrika wameona kwamba migogoro na vita ni sababu kubwa zinazosababisha umaskini barani Afrika.

Naibu mkuu wa Chuo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Cameroon Bw Stephane Ngwanza amesema mfumo wa kisiasa wenye utulivu unafanya kazi kubwa katika kuendeleza uchumi na kuondokana na umaskini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu