Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo amezungumza na wanahabari kuhusiana na hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyeko katika hospitali ya Narobi nchini Kenya kwa matibabu.
Mh,Mbowe amesema Mh,Lisu anaendelea vizuri na kuimarika lakini amesema Mh,Lissu amefanyiwa upasuaji mara kumi na saba lakini pia amepewa damu nyingi kuliko mgonjwa yeyote hapo hosptalini tangu miaka ishirini iliyopita Lakini pia Mh,Mbowe amesema mashine alizokua akizitumia katika kuendesha ama kusapoti mwili wake zimeondolewa na sasa anatumia wilchair.
Kwa upande mwingine Mh.Mbowe amewashukuru madaktari wote toka Tanzania na Kenya waliookoa maisha ya Mh,Lissu,pia amesema Hosptali ya Kenya imefikisha awamu ya pili ya matibabu huku baada ya hapo itafanyika awamu ya tatu ya matibabu nay a muda mrefu katika kuimarisha afya na kumtibu Mh.Lissu ambapo awamu hiyo itafanyika nje ya Tanzania na Kenya kwa sababu ya kiusalama.
