Agizo la Rais Dr John Pombe Magufuli alilolitoa jana kuhusu wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji, limeibua maswali bungeni mapema leo.
Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chadema Peter Msigwa katika swali la nyongeza, amesema agizo hilo linakinzana na sheria ya mazingira na kutaka kujua wao wamsikilize nani kati ya rais na waziri husika.
Swali hilo lilijibiwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kangi Lugola, kisha likatiliwa mkazo na waziri mwenye dhamana January Makamba.
Kutokana na kile alichokisema Msigwa kuwa Rais anafanya upendelea kanda ya ziwa, waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba alisimama na kulizungumzia hilo.
