Mbunge aomba Bunge kujadili Tatizo la Panya Road.

Mbunge wa viti malaum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
CCM Bahati Ndingo,leo amesimama Bungeni na kutoa hoja ya
kutaka Bunge liahirishwe kwa muda na lijadili usalama wa Raia,
kufutaia matukio ya yanayofanywa na Kikundi cha Panya Road,
kinachodaiwa kuuawa mtu mmoja usiku wa kuamkia leo Jijini
Dar es salaam.


Imeelezwa Vijana hao zaidi ya 30 wamemsababishia umauti
Binti aliyefahamika kwa jina la Maria Baso mwenye umri wa
miaka 24 katika tukio la uvamizi huku wengine 2 wakijeruhiwa.
Tukio hilo linadaiwa kutokea eneo la Kawe Mzimuni jijini Dar
es Salaam,ambapo vijana hao pia wamepora vitu mbalimbali
ikiwemo simu na fedha.

Sasa Sakata la Vijana hao limefika Bungeni kwa Mara nyingine
na mtaa wa mastory tumeinasa sauti ya Mbunge Bahati Ndingo
akitoa hoja hiyo.

Baada ya kutoa hoja hiyo Spika wa Bunge Dkt Tulia Akson,
akaitolea ufafanuzi lakini Vilevile akatoa Maagizo kwa Serikali
kushughulikia suala hilo kwa haraka.

Exit mobile version