Mbunge CCM ashikiliwa kwa kuua.

In Kitaifa

Jeshi la Polisi mkoa wa Singida linamshikilia mbunge wa Manyoni, Daniel Mtuka (CCM) kwa tuhuma za kumuua mwanafunzi wa darasa la kwanza kwa kumgonga na gari alipokuwa akijaribu kuvuka barabara mkoani hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Debora Magilingimba, Mbunge huyo  aliyekuwa akisafiri na gari lake aina ya Toyota Prado alimgonga mwanafunzi huyo na kwamba uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wake wa kutochukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.

Kamanda Magilingimba alisema kuwa jeshi hilo linamshikilia Mtuka tangu jana kutokana na tukio hilo na watamfikisha mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheria.

Aliongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Manyoni kwa uchunguzi wa madaktari.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu