Bunge la kumi nambili mkutano wa 7 kikao cha 20 linaendelea
jijini Dodoma,ambapo wabunge wamepata fursa za kuuliza
maswali na Serikali kutoa majibu pia kuchangia makadirio ya
bajeti kwa mwaka wa fedha 2022-2023.
Moja ya jambo ambalo pengine hukuwa ukifahamu ni sababu ya
kuwepo kwa kiti cha pili pembeni ya kiti cha waziri mkuu pale
Bungeni.
Leo Spika wa Bunge Dkt Tulia Akson ametolea ufafanuzi wa
kiti hicho na kuwataka wabunge kufahamu kuwa kila mbunge
anaruhusiwa kukikalia kiti hicho sio kwa zaidi ya dakika tatu tu.
