MBUNGE wa jimbo la Dodoma Mjini ANTHONY MAVUNDE leo kaamezindua mifumo maalum ya vipimo vya kibaiolojia BIOMETRIC SYSTEM na CCTV Cameratika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma utakaosaidia kuboresha huduma za afya na kupunguza kero za wananchi.
Akizungumza katika uzinduzi huo MAVUNDE ambaye pia ni naibu waziri wanchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu amesema kama mbunge wa jimbo hilo kazi yake kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na uwepo wa mifumo hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kupata huduma bora sambamba na kutambua uwajibikaji wa wafanyakazi.
Aidha itawezesha kujua watumishi wa hospitali hiyo muda wanaoingia kazini na muda wanaotoka ,ili kuwezesha kutowanyima stashiki zao hasa pale wanapotekeleza majukumu yao katika muda wa ziada.
Uzinduzi huo umehusisha CCTV Camera 4 zilizofungwa na mfumo wa Biometric mmoja vyote kwa pamoja vikiwa na gharama ya shilingi milioni 10 fedha ambazo zimetoka katika ofisi ya jimbo.
Akitoa shukrani katika uzinduzi huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo dokta CAROLINE DAMIAN ,amesema tangu kufungwa kwa mfumo huo ufanisi wa kazi umeongezeka na malalamiko kutoka kwa wananchi yamepungua.
Kutokana na mafanikio hayo ameomba upatikanaji wa CCTV Camera zaidi ili kufikia idadi ya camera 100 na kuongeza idadi ya mfumo wa Biometric kuweza kufikia 3.
