Mchungaji aliyepata almasi inayotajwa kuwa miongoni mwa almasi zenye ukubwa zaidi duniani, sasa anasema hatarajii chini ya dola milioni 50 za Marekani.
Hii ni baada ya kutofika bei iliyotarajiwa kwenye mnada nchini Sierra Leona, kulingana na shirika la AFP
Bei ya juu zaidi ya dola milioni 7.8 kwenye mnada huo, imetoka kwa raia wa Uingereza, anayeishi Antwerp na soko kubwa la Almasi Uropa, lililoko Ubelgiji, ambapo mnada ujao utaandaliwa wiki chache zijazo.
Hata hivyo, bei kamili ya Almasi hiyo, ambayo ndio bei yake ya mwisho, imewekwa na serikali ya Sierra Leone, na inasalia kuwa siri.
Mnamo mwezi Mei mwaka uliopita, kampuni ya kuzalisha almasi ya Lucara, iliuza almasi yenye uzani wa Karat 813 kwa dola milioni 63 katika mnada wa kipekee mjini London.
