MCT kuwachulia hatua wanaonyanyasa wanahabari…

Baraza la habari Tanzania MCT limesema kuwa, litawachukulia hatua ikiwamo kuwafikisha mahakamani, wote watakaowazuia na kuwanyanyasa waandishi wa habari wakiwa kwenye majukumu yao.
Akizungumza leo wakati wa siku ya kimataifa ya kupinga jinai dhidi ya wanahabari, katibu mtendaji wa MCT Kajubi Mukajanga amesema kuwa, baraza hilo haliridhishwi na hali ya uhuru wa habari iliyopo hivi sasa.
Amesema hatua hiyo inatokana na kukithiri kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya viongozi wa serikali, pamoja na upindishwaji wa sheria unaolenga kuwakandamiza wanahabari.

Exit mobile version