Mdahalo wa tatu na wa mwisho wa wagombea sita wa kiti cha urais wa awamu ya 12 ,katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, utafanyika leo.
Mdahalo huo utarushwa hewani kwa njia ya moja kwa moja, kupitia Televisheni ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu la Iran IRIB.
Mdahalo wa leo utajikita katika masuala ya uchumi, baada ya midahalo miwili iliyopita ambayo ilijumuisha masuala ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
