Meya wa jiji la Arusha Kalisti lazaro ametoa siku tatu kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, kutoa taarifa sahihi ya michango ya rambi rambi ya wafiwa kwa familia 35 zilizo poteza ndugu zao, katika ajali ya basi aina ya costa iliyotokea eneo la Rhotia wilayani karatu.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Meya amesema amefikia kutoa taarifa kwa vyombo vya habari, kutokana na usumbufu mkubwa anao upata kutoka kwa wananchi kufika ofisini kwake ,na wengine kumpigia simu mara kwa mara kuuliza kuhusu ugawaji wa fedha hizo huku ,wengine wakimtumia jumbe za mpesa wanazo tumiwa fedha za rambi rambi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo juzi wakati akiwaaga majeruhi wa ajali amesema kuwa ,tarifa ambazo zimekua zikisambazwa katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye kutoa taarifa za fedha walizo gawa kwa familia za wafiwa na kudaiwa kuwa fedha hizo hazija wafikia walengwa sio za kweli na kwamba ni za kisiasa, na kuwataka wananchi kuzipuuzia taharifa hizo kwani azina ukweli
