Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro ameunga mkono utumbuaji wa rais John Pombe Magufuli na kutaka rais huyo kuwashughulikia viongozi wa awamu ya tatu na ya nne kwa uzembe wa kukubali mchanga wa dhaabu kuuzwa nje kama njugu na kusababishia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.
Akizungumza katika baraza la madiwani Meya Kalisti amesema haiwezekani makatibu wa wizara ya nishati wakaachwa pamoja na viongozi wao wakati waliruhusu uvujaji wa mabilioni katika upakiaji wa mchanga kusafirishwa nje.
