Migogoro ya Ardhi yapungua Morogoro.

Wakazi wa Kata ya Mngazi Wilaya ya Morogoro, wamesema migogoro ya ardhi iliyokuwa imekithiri katika maeneo yao, imepungua kutokana na ushirikiano wao.

Wananchi hao wamesema hayo wakati wakizungumza na waandishi wa habari, walioukuwa katika kata hiyo kufahamu namna migogoro ya ardhi, inavyotatuliwa maeneo ya vijijini.

Wamesema migogoro ya ardhi iliyokuwa inasumbua katika eneo lao, ni pamoja na mipaka, mashamba ya urithi na baadhi ya viongozi wa vijiji, kuuza maeneo bila ya kuwashirikisha wananchi.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Vigolegole Octavian Kobelo, amesema hivi sasa kesi za ardhi katika baraza la ardhi kata, zimepungua kwa kiasi kikubwa.

 

 

 

 

Exit mobile version