Wana akiolojia wamegundua kaburi lenye miili ya mwanamke na watoto wake, waliokuwa wamehifadhiwa karne kadhaa zilizopita.
Kaburi hilo linaloaminika kuwa la karne ya 16 hadi 11 kabla ya Kristo, lilipatikana karibu na mji wa Luxor kilomita 70 kutoka Cairo.
Kati ya vifaa vilivyopatikana ndani ya kaburi hilo, ni sanamu ya mfua viuma Amenemhat akiketi kando na mke wake.
Kulingana na wana akiolojia hao, mama huyo alifariki akiwa na miaka 50, na uchunguzi ulionyesha kuwa alifariki kutoka na ugonjwa wa mifupa.
Watoto wawili wa kiume walikuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 30 na walikuwa wamehifadhiwa katika hali nzuri.
