Serikali imetoa Rai kwa wataalamu na wabunifu wa TEHAMA
hasa wanawake na Vijana,kuwa tauari kupokea Teknolojia mpya
zinazoibuka kwa kasi na kuwa na hamasa ya kubuni mambo
makubwa ya kisayansi,kupitia changamoto zilizopo katika jamii,
hatua itakayokuza mkakati wataifa wa ujenzi wa uchumi
jumuishi wa kidigital nchini.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu mkuu Wizara ya Habari
Selestine Kakele,alipokuwa akizungumza na wadau wa Tehama
katika kongamano linalofanyika jijini Dar es salaam.
