Miradi 9 ya barabara kuzinduliwa na Rais Magufuli.

In Kitaifa
RAIS John Magufuli anatarajiwa kuzindua miradi tisa ya barabara na uwanja wa ndege ambayo itaunganisha mikoa ya Ukanda wa Kati na Magharibi nchini na nchi jirani kwa barabara za lami katika kuchochea harakati za maendeleo ya uchumi wa viwanda.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Ujenzi, Joseph Nyamhanga alisema jana kwa simu kwamba uzinduzi wa miradi hiyo utafanyika katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kuanzia kesho hadi 25, mwaka huu.
Nyamhanga amesema ufunguzi wa Barabara ya Kigoma – Biharamulo – Lusahunga yenye urefu wa kilometa 154 utafanyika Biharamulo Mjini mkoani Kagera kesho ,huku uzinduzi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Nyakanazi – Kibondo yenye urefu wa kilometa 50 utafanyikia Kakonko mkoani Kigoma, Julai 21.
Ameeleza kuwa uzinduzi wa Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kidahwe –Kasulu yenye urefu wa kilometa 63 utafanyika Kasulu Mjini mkoani Kigoma, Julai 21 ambako pia ufunguzi wa barabara ya Kaliua – Kazilambwa yenye urefu wa kilometa 56 utafanyika Julai 23 Kaliua Mjini mkoani Tabora.
Aidha, Katibu Mkuu alieleza kuwa ufunguzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora utafanyika Julai 24 na ufunguzi wa mradi wa Manyoni – Itigi – Chanya wenye urefu wa kilometa 89.3 utafanyika Itigi mkoani Singida Julai 25, mwaka huu.
Aidha, amesema ufunguzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha miundombinu ya viwanja vya ndege na usafiri wa anga nchini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

MAJALIWA ATOA RAI KWA WAMILIKI WA MALORI KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa malori nchini wawajali madereva na wahudumu wa magari hayo ikiwa ni pamoja

Read More...

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu