Tanzania na Misri zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii, katika maeneo makuu kumi.
Maeneo hayo ni pamoja na kuimarisha uhusiano, ulinzi na kujenga kiwanda kikubwa cha nyama, pamoja na kiwanda cha dawa nchini.
Hata hivyo suala la matumizi ya maji ya Mto Nile halijapatiwa muafaka, na mazungumzo yanaendelea kuwezesha matumizi yenye faida ya mto huo kwa nchi zote zinazohusika.
Aidha Misri imempongeza Rais Magufuli kwa utawala mzuri, kwa namna anavyopambana na rushwa na ufisadi, na kufafanua kuwa nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania.
