Mkataba wa amani Mali ndio Muarobaini kwa sasa-Lacroix

In Kimataifa

Kuongeza kasi ya utekelezaji wa mkataba wa amani nchini Mali ndio njia pekee ya kumaliza sintofahamu ya kiusalama na kibinadamu inayoendelea hivi sasa.

Hiyo ni sehemu ya ujumbe wa mkuu mpya wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix wakati kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana leo katika kikao chake cha kila baada ya miezi mitatu kujadili amani na usalama katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Amesema ingawa kuna mafanikio kama vile mkutano wa tarehe Pili mwezi huu kuhusu mashauriano na maelewano ya kitaifa yaliyotoa fursa ya kipekee kwa wananchi kupaza sauti zao, bado kuna kasi haitoshi.

(Sauti ya Lacroix)

“Kwa ujumla kasi ya utekelezaji iko taratibu. Mkakati wa kitaifa kuhusu marekebisho katika sekta ya usalama bado haujakamilika. Vigezo vya kujumuisha wapiganji kutoka vikundi vilivyosaini makubaliano hayo bado havijawekwa na vituo vinane vilivyojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA bado ni vitupu.”

Bwana Lacroix amesema marekebisho ya muundo wa jeshi la serikali ni muhimu na kwamba bila hatua hiyo..

(Sauti ya Lacroix)

“Ukosefu wa ufafanuzi juu ya marekebisho ya miundo ya taasisi, ni kikwazo nchini humo na hausaidii kujenga kuaminiana baina ya pande kinzani. Hali hii inachochea mazingira ya mgawanyiko wa kisiasa na hivyo kufanya kazi yetu ya kusaka amani kuwa ngumu zaidi.”

Kuhusu usalama amesema bado hali si shwari na vikundi vilivyojihami vimeendelea kutekeleza mashambulizi ambapo amesisitiza umuhimu wa utekelezaji wa mkataba amani ili kufungua fursa ya suluhu ya kudumu ya mzozo wa Mali.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu