Mkataba wa Kocha ‘Kinnah Phiri’ na Mbeya City haujavunjwa.

 

Klabu ya Mbeya City FC Jana September 13 mwaka huu ilifikia makubaliano ya kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha mkuu wake Mmalawi Kinnah F. Phiri.

Kocha huyo leo ameibuka na kusema kuwa bado hawajavunja mkataba na mkataba wake utavunjwa baada ya kulipwa pesa zake ambazo anadai kutoka katika klabu hiyo.

‘’Mkataba wanngu haujavunjwa na utavunjwa mara baada ya kunilipa deni langu ambalo nawadai na wamesema mwezi November wataandika barua kwenda TFF ili niweze kulipwa pesa ninazo idai klabu’’ amesema Kinnah Phiri.

Kikao hicho kilichokaa jana kilikuwa ni muendelezo wa vikao kadhaa baina ya pande hizi mbili toka mwezi julai mwaka huu. Baada ya majadiliano marefu pande zote mbili walikubaliana kutoendelea na makubaliano yao ya hapo awali.

Sababu kubwa ya kutoendelea na makubaliano baina ya Phiri na klabu ya Mbeya City ni matokeo mabaya ya timu ya msimu uliopita 2016/2017 ambayo yaliipunguzia klabu uwezo mkubwa wa kuhimili mahitaji yake ya msingi baada ya wadhamini waliotarajia kuingia kushindikana na wadhamini waliopo kupunguza kiwango cha udhamini wao kutokana na matokeo hayo yasiyoridhisha.

Pamoja na hayo Klabu ya Mbeya City ilimshukuru Kocha Phiri kwa mchango wake muhimu katika timu hiyo na kuweka wazi kuwa kwa sasa timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Mohamed Kijuso.

Exit mobile version