Kesho tarehe 19 na kesho kutwa tarehe 20 kutakua na mkutano maalum kuhusiana na Usafiri wa anga utakaolenga mambo mbalimbali ya sekta ya anga hapa nchini yakiwamo kuhakikisha wanafikia malengo ya uchumi wa kati na kujitathimini wapi walipo na wapi wanaelekea zikiwamo na changamoto zinazowakabili.
Lakini pia Mkurungenzi huyo ameeleza mgeni rasmi katika kikao hicho ni Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Mh.Makame Mbarawa,Lakini pia watakuepo wataalamu mbalimbali wataoelezea mambo mengi kuhusiana na usafiri wa Anga.
