Mkurugenzi wa Uturuki wa Shirika la Kutetea haki za Binaadamu Amnesty International, Taner Kilic, amekamatwa na mamlaka za usalama nchini humo kwa madai ya kuwa na mafungamano na vuguvugu la kiongozi wa kidini Fethullah Gülen.
Serikali ya uturuki inawalaumu wafuasi wa Gulen kwa kuchochea jaribio la mapinduzi la Julai 15 mwaka jana, lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 250.
Tokea wakati huo Uturuki imekuwa katika hali ya hatari. Maelfu ya watu wamekamatwa au kusimamishwa kazi zao serikalini, mara nyingi bila ya kuwepo ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha matukio ya kuipinga serikali.
