Mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki IGAD watakutana siku ya Jumatatu jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili hali ya usalama nchini Sudan Kusini

Mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki IGAD watakutana siku ya Jumatatu jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili hali ya usalama nchini Sudan Kusini.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn ambaye pia ni Mwenyekiti wa IGAD, ataongoza mkutano huo kujaribu kutafuta mwafaka kati ya serikali na makundi ya waasi.

Mkataba wa kisiasa uliotiwa saini kati ya rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar mwaka 2015, ulivunjika miezi kadhaa tu baada ya kuanza kutekelezwa huku kila upande ukilaumiana.

Mkutano huo utajadili namna ya kusitisha mapigano yanayoendelea lakini pia namna ya kuwasadia maelfu ya watau ambao wanaohitaji misaada ya kibinadamu  kama chakula, dawa na maji safi ya matumizi.

Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya Milioni 3 wameyakimbia makwao huku wengine Milioni 2 wakiwa wakimbizi wa ndani. Maelfu ya wakimbizi wamekimbilia nchini Kenya, Sudan na Uganda walikopewa hifadhi.

Haijafahamika vema  ikiwa kiongozi wa waasi Riek Machar ambaye anaishi nchini Afrika Kusini atahudhuria mkutano huo.

Mwezi Mei rais Salva Kiir, alitangaza kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa na kusitisha mapigano, mazungumzo ambayo yamesusiwa na kulaaniwa na upinzani.

Exit mobile version