Chuo kikuu cha Arusha kimemsimika mkuu mpya wa chuo
hicho wakati wa mahafali ya 16 ambayo yamefanyika chuoni
hapo.
Mkuu aliyeachia nafasi hiyo ni Dkt na Prof Godwin Lekundayo
na aliyesimikwa kuwa mkuu mpya wa chuo hicho ni Dkt na Prof
Mark W Malekana.
Mgeni rasmi katika Mahafali hayo ambaye ni mbunge wa bunge
la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Prof Shukran Manya,
amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kuwa na
mawazo yaliyofunguka kutoa miongozo ya kutatua changamoto
ya ajira,na pia kuwa wavumilivu wakati wakiendelea kusubiri
Ajira.
Mahafali hayo ni ya 16 na waliofanikiwa kuhitimu jumla yao ni
wanafunzi 310 kwa ngazi tofauti.
