Alpha Conde, ambaye ni rais wa Guinea amesema kilichotokea Zimbabwe bila shaka ni “wanajeshi kujaribu kuchukua mamlaka kwa nguvu”.
Mkuu huyo wa Umoja wa Afrika (AU) ametoa wito kwa jeshi kukomesha wanalofanya – jambo ambalo amesema “linaonekana kama mapinduzi ya serikali”, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Hilo linakinzana na msimamo wa jeshi la Zimbabwe ambalo limesisitiza kwamba halijatekeleza mapinduzi ya kijeshi, bali linajaribu kuwaondoa “wahalifu” wanaomzingira Rais Mugabe.
