Mkuu wa Benki Kuu ya Gambia aliyekuwa akihudumu wakati wa utawala wa Yahya Jammeh, Amadou Colley, amefutwa kazi.
Hakuna sababu zozote zilizotolewa kuhusiana na kufutwa kwake.
Bw Colley mwenyewe ameambia Reuters kwamba hajui ni kwa nini ameachishwa kazi.
Bw Colley alihudumu chini ya Rais Jammed ambaye alituhumiwa na baadhi ya maafisa wa serikali mpya kwamba alipora mamilioni ya dola kutoka kwa hazina ya serikali wakati wa utawala wake wa miaka 22.
Tangu achukue madaraka Januari, Rais Adama barrow amekuwa akiwafuta kazi na kuteua maafisa wapya katika nyadhifa zenye ushawishi serikalini.
Bw Barrow alimshinda Jamme kwenye uchaguzi mkuu Desemba, ingawa rais huyo alikubali kuondoka wiki kadha baadaye baada ya kushinikizwa na jamii ya kimataifa.
Kwa sasa, Jammeh anaishi uhamishoni Equatorial Guinea
