Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amefungua majengo mawili ya ofisi ya usalama barabarani huku akiwahimiza askari wa jeshi hilo Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya kufanya kazi kwa weledi, uwaadilifu, kujituma na kuwa na mahusiano na kushirikiana na wananchi katika ulinzi wa taifa na kupambana na uhalifu.
Akizungumza na askari hao wa Polisi wa Tarime/ Rorya katika hafla ya uzinduzi wa majengo hayo yaliyojengwa kwa gharama zaidi ya Sh milioni 40 sirro amewataka askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria bila kumuonea mtu.
Kamanda wa Polisi wa Tarime/ Rorya, Henry Mwaibambe amesema majengo hayo yamegharimu milioni 21 laki tisa na sabini na nane elfu, wakati jengo la michezo ambalo halijakamilika linatarajiwa kukamilika kwa zaidi ya Sh milioni 25.
Aidha amezitaja changamoto nyingine zinazokabili Kikosi cha Usalama Barabarani ni magari, pikipiki za kufanya doria ili kudhibiti vitendo vya makosa ya barabarani.
