Mkuu wa mashtaka nchini Sweden ameamua kuachana na mashtaka ya ubakaji dhidi ya mwanzilishi wa mtandao wa uchunguzi wa Wikileaks, Julian Assange.

In Kimataifa

Mkuu wa mashtaka nchini Sweden ameamua kuachana na mashtaka ya ubakaji dhidi ya mwanzilishi wa mtandao wa uchunguzi wa Wikileaks, Julian Assange.

Marianne Ny amesema amefikia uamuzi kwa sababu ameshindwa kumpa Assange taarifa ya maandishi kuhusu mashtaka yanayomkabili.Assange mwenye umri wa maika 45, amekuwa akiishi katika Ubalozi wa Ecuador jijini London kuanzia mwaka 2012.

Wakili wake, Per Samuelson, amesema uamuzi huo wa kiongozi wa mashtaka ni ushindi mkubwa kwa Assange.

Raia huyo wa Australia amekuwa akisema hawezi kwenda nchini Sweden kwa sababu ana hofu kuwa atasafirishwa kwa nguvu kwenda nchini Marekani, anakotuhumiwa kuvujisha siri za serikali.

Hata hivyo, Polisi jijini London wanasema watamkamata Assange ikiwa ataondoka katika Ubalozi huo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu