Mkuu wa mkoa wa ARUSHA Mrisho Gambo atembelea kituo cha kupozea umeme cha Gridi -Njiro

Mkuu wa mkoa wa ARUSHA Mrisho Gambo ametembelea kituo cha kupozea umeme cha Gridi -Njiro ambacho ndicho kinapoza umeme kabla haujasambazwa kwenda maeneo mbalimbali kwa ajili ya matumizi.

Akitoa taarifa mbele ya mkuu wa mkoa msimamiziwa uthibiti mapato Tanesco Mkoa wa Arusha Fatuma Boutte amesema kuwa mpaka sasa kuna miradi miwili ya Upanuzi ya kuongeza nguvu ya umeme na kuimarisha miundombinu iliyokuwa imechakaa nakuondoa mfumo ukitumika zamani.

Kwa upande wa Garama za miradi hiyo Boutte ameleza kuwa ni shilingi Bilioni 78 ambazo ni fedha kutoka benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB )pamoja na nyingine nyingine bilioni 50 kutoka benki ya Dunia (WB).

Akizungumzia changamoto wanazopata shirika la TANESCO ni uwizi wa miundombinu ya umeme Hasa Nyaya na vyuma chakavu ,wateja na wasio wateja kujiunganishia umeme ,pamoja na kutokuwa na mipango miji inayotenganisha maeneo ya  viwanda ili kusambaza umeme.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Mkuu wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo amepongeza shirika la umeme TANESCO kwa kazi nzuri walioifanya kwani wametimiza adhma ya Raisi Magufuli ya Tanzania ya Viwanda huku akiwahakikishia umemewa kutosha wawekezaji wanaotaka kuja kuanzisha viwanda mkoani Arusha .

Hata hivyo amemuagiza Meneja Tanesco Arusha kuhakikisha anafuatilia watu wote wanaodaiwa kulipa madeni yao bila kujali sekta binafsi au sekta za Umma kwasababu kufanya hivyo kutafanya shirika hilo kufanya kazi yake vizuri.

Kufuatia tabia ya changamoto wanayoipata TANESCO ya wizi wa umeme Gambo ameliagiza jeshi polisi linawasaka popote walipo na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wanaojihusisha na tabia ya uwizi wa nyaya za umeme kwa kupitia pia wananchi kutoa taarifa za wanaohusika

 

 

Exit mobile version