Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Robert Gabriel, ameagiza watu waliyosababisha uharibifu wa samani za mamilioni ya fedha katika Hospitali ya Wilaya ya Magunga, wachukuliwe hatua za kisheria.
Gabriel amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo, na kukuta samani mbalimbali za mamilioni ya shilingi, zikiwa zimetelekezwa maeneo yasiyo rasmi.
Kutokana na hali hiyo alionyesha kutofurahishwa na kumtaka Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Dk Frank Chiduo kutoa maelezo, ambayo hata hivyo hayakumridhisha.
Kwa upande wake katibu wa Afya Dk Frank Mhilu katika maelezo yake, amesema inawezekana vifaa hivyo viliwekwa eneo hilo baada ya kuonekana kuwa vibovu.
