Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh Beno Malisa amewatoa hofu wakazi wa Wilaya ya Mbeya kutokana na Kuwepo kwa taarifa ya uhaba wa mafuta katika baadhi ya Maeneo Mkoani Mbeya.
Akitembelea katika baadhi vituo vya Mafuta Jijini Mbeya na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya dc) huku akiambatana na Meneja wa wa EWURA Mkoa wa Mbeya Dickson Semkuyu , Mh. Malisa amejionea hali halisi ya upatikanaji wa huduma ya mfuta na kubainisha kuwa hakutokuwa na Changamoto kubwa kuhusu uhaba wa mafuta na kuwataka Wafanyabishara, watumiaji wa Vyombo vya moto na Wakazi wa Mbeya kuwa watulivu Huku jitihada za dhati zikichukuliwa kutatua changamoto hiyo.
