Mkuu wa Wilaya ya Mbulu asuluhisha mgogoro wa muda mrefu.

In Kitaifa

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga, amesuluhisha mgogoro wa muda mrefu wa viongozi wa kanisa la KLPA waliokuwa wanagombania mali za kanisa na kusababisha kanisa hilo kufungwa kwa miezi tisa.

Kwa muda wote wa mgogoro huo, waumini wa kanisa hilo walikuwa wanasali nje kutokana na kanisa hilo kufungwa.

Akizungumza baada ya kuwapatanisha viongozi hao, Mofuga alikemea vikali kitendo cha baadhi ya viongozi wa dini wanaoanzisha migogoro na kuwasumbua waumini wao.

Alisema kitendo cha viongozi wa dini kuzua malumbano sababu ya mali ya kanisa na kusababisha mgogoro siyo jambo jema hivyo wajipange upya na kuachana na tatizo hilo.

Alisema kwa muda wote wa miezi tisa waumini wamesali nje ya kanisa baada ya viongozi wengine kujiengua na kusababisha kugombea mali za kanisa.

“Tumefanikiwa kumaliza mgogoro huu sasa tumieni nafasi hiyo kwa kujiimarisha ninyi viongozi wenyewe na waumini wenu ili mzidi kupiga hatua nzuri mbele,” alisema Mofuga.

Aliwataka viongozi na waumini wa kanisa hilo kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kuhakikisha anaipeleka Tanzania kwenye neema ya uchumi wa kati na siyo kuanzisha upya migogoro.

“Rais Magufuli ni kama Mussa alivyokuja kuwakomboa jangwani wana wa Israel, sasa na ninyi viongozi na waumini, muombeeni kwa Mungu huku mkifanya kazi kwa bidii na siyo mgogoro,” alisema Mofuga.

Waumini wa kanisa hilo walipongeza kitendo cha mkuu wa wilaya hiyo kusuluhisha mgogoro huo ambao ulichukua miezi tisa na kusababisha wao kusali nje.

Mmoja kati ya waumini hao John Qwari alisema jitihada za mkuu huyo wa wilaya zimesababisha hivi sasa upendo urudi upya kama awali kwenye kanisa hilo.

“Mkuu wa wilaya yetu tumezoea kumuona akitatua migogoro mingi hasa ya ardhi, lakini sasa amefanikiwa kutatua mgogoro wa kanisa letu uliochukua muda mrefu tunamshukuru sana Mungu ambariki,” alisema Qwari.

Katibu Mkuu wa Parish ya Mbulu, Mathew Tsuut alisema mgogoro umemalizika hivyo waumini na viongozi wanapaswa kusahau yaliyopita na kuganga yajayo.

Tsuut alisema ni muda mrefu kulikuwa na mgogoro baina ya viongozi na viongozi hadi kusababisha kanisa hilo kufungwa kwa muda wa miezi tisa na waumini wao kusali nje ya kanisa hilo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu