Emmerson Mnangagwa, kwa jina la utani The the crocodile”, ameanza hotuba yake kama rais wa Zimbabwe.
”Nahisi furaha sana kwa uamuzi wa chama cha Zanu PF kunialika kuhudumia taifa letu la Zimbabwe kama rais na kamanda mkuu wa majeshi kuanzia leo”.
”Sina ujuzi wa kazi hii lakini nitawahudumia wananchi wote bila upendeleo wa rangi ama kabil”a. Amemsifu Robert Mugabe kwa kupiginia uhuru huku akisema kuwa alichukua uongozi wakati mgumu .
Amesema kuwa licha ya makosa yaliofanywa na Mugabe ni muhimu kukubali na kutambua mchango wake kuhusu ujenzi wa taifa. ”Kwangu mie bado ni rafiki mkubwa”.
