Mosscow:Ajali ya moto hospitali yawaua wagonjwa 5 wa virusi vya corona

Ajali ya moto katika hospitali ya St George iliyoko mjini St. Petersburg imewaua wagonjwa watano wa virusi vya corona waliokuwa kwenye mashine za kupumulia. Moto huo umezuka katika wadi ya wagonjwa mahututi na baadae kuzimwa ndani ya nusu saa. Shirika la Interfax limeripoti kuwa chanzo cha moto huenda ni hitilafu katika mashine hizo. Polisi mjini St. Petersburg ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Urusi wameanza uchunguzi kubaini chanzo cha ajali. Wakati huo Urusi, leo imeripoti kesi mpya 10,899 za virusi vya corona katika kipindi cha saa 24, na kufanya idadi jumla ya maambukizi kufikia 232,243. Kituo kinachoshughulikia janga hilo kimesema idadi ya vifo nayo imeongezeka kwa watu 107 na kufikia 2,116.

Exit mobile version