Mpigapicha ashinda kesi kuhusu selfie ya tumbili.

Mpiga picha mmoja ameshinda kesi iliyodumu kwa miaka miwili, dhidi ya kundi la kutetea haki za wanyama kuhusu haki za kumiliki picha ambayo ilipigwa na tumbili.

Tumbili kwa jina Naruto alidaiwa kujipiga picha hiyo katika msimu mmoja Indonesia mwaka 2011, alipoichukua kamera iliyokuwa inamilikiwa na David Slater kutoka Monmouthshire.

Majaji nchini Marekani wamesema kuwa,tumbili huyo hangekabidhiwa haki miliki ya picha hiyo.

Watetezi wa haki za wanyama kutoka kwa kundi la People for the Ethical Treatment of Animals (Peta), ambao walikuwa wamewasilisha kesi hiyo kwa niaba ya tumbili huyo, walisema mnyama huyo anafaa kufaidi kwa njia fulani.

Kesi hiyo ya Peta “kwa niaba ya tumbili” imetupiliwa mbali lakini Bw Slater amekubali kutoa asilimia 25 ya mapato yatakayotokana na picha hiyo siku zijazo.

Bwana Slater alidai kuwa ilimchukua siku tatu kuruhusiwa kuwakaribia tumbili hao.

Exit mobile version