Mpina atangaza vita dhidi ya uvuvi haramu.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, amezitaka halmashauri ambazo shughuli za uvuvi zinafanyika kutenga fedha ili kuweza kupambana na uvuvi haramu.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya kujionea dhana mbalimbali zinazotumiwa na wavuvi haramu, zilizokamatwa na kikosi maalumu cha kupambana na uvuvi haramu.

Waziri Mpina amewataka Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Mkurugenzi, waanze kutembea na barua za kuwafukuza kazi watumishi wanaoshirikiana na wavuvi haramu.

Msikilizaji kama hukuwa ukifahamu ni kwamba madhara yanayosababishwa na Samaki waliovuliwa kwa kutumia mabomu, ni pamoja na magonjwa ya tumbo na saratani.

Exit mobile version