WIZARA ya Elimu, Sayanasi, Teknolojia na Ufundi imefanya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu ya waalimu, wenye Thamani ya Bil. 83 utakaotekelezwa katika vyuo vyote vya ualimu vya serikali.
Katika vyuo vya serikali vya elimu ya ualimu hapa nchini vimeonekana kubaliwa na changamoto mbalimbali ,kama vile miundombunu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na uchakavu wa nyumba za waalimu.
Hata hivyo kupatikana kwa fedha hizo kunakuwa ni neema kuwa wakufunzi pamoja na wanafunzi wa vyuo hivyo, baada ya wizara hiyo kuelekeza fedha hizo katika kukabilina na changamoto hizo katika vyuo 35 vya ualimu vya serikali.
Akizindua mradi huo mbele ya wakuu vya vyuo hivyo mjini Dodoma katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi, teknolojia na ufundi Prof. SIMON MSANJILA amesema kuwa mradio huo wa bil. 83 umefadhiliwa na Serikali ya Canada.
Naye Mkurugenzi msaidizi mipango na bajeti ambaye pia msimamizi wa mradi huo GERALD MWELI, amesema kuwa lengo la kutoa mafunzo kwa wakuu hao wa vyuo ni kuwafanya wasimamie miradi kama ya kwao, tofauti na ilikuwa hapo awali.
Mradi huo unatarajiwa kuanza wiki ijayo na utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu huku matarajio yakiwa ni kuukamilisha kabla ya muda huo kufika
