Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka waajiri wa
wafanyakazi katika sekta binafsi kufata maelekezo ya serikali
kuhakikisha watumishi wote kima chao cha chini kinaanzia shs laki
tatu na nusu kama ambavyo serikali imesema.
Gambo ameyasema hayo jijini Arusha katika viwanja wa Sheikh
Amri Abed ,wakati wa maazimisho ya siku ya wafanyakazi na kusema changamoto kubwa imewalenga wafanyakazi wa sekta
binafsi ,ambao mishahara yao kima cha chini ni shilingi laki moja tofauti na
maelekezo ya serikali ambapo kima cha china kinaanzia laki tatu na
nusu.
Aidha Gambo amesema ni kosa kwa mtumishi yoyote kufanyishwa kazi na mtu
yoyote au kampuni yoyote, bila kuwa na mikataba ya ajira hivyo
watumishi wa idara ya kazi mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha
wanapitia waajiri wote wa serikali na sekta binfsi, kuhakikisha kwamba
wanawapatia mikataba ya ajira watumishi wao na wale waajiri wote na
ambao hawatafanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Kuhusu kutokupanda kwa mishahara Gambo amesema changamoto hiyo
imesababishwa na wafanyakazi waliokua wanatumia vyeti visivyokuwa
sahihi na wafanyakazi hewa, na amewahakikishia watumishi wote wa mkoa
wa Arusha kuwa watumishi wote wanaostahili kupanda daraja
watapandishwa daraja na wanaodai maslahi yao , watapewa baada ya
kukamilika kwa zoezi la kuwabaini wafanyakazi hewa na wasio kuwa na
vyeti halali.
