Mshambuliaji mwenye bunduki amewafyatulia risasi wabunge wa chama cha Republican waliokuwa katika mazoezi kujiandaa na mchezo wa hisani wa baseball, na kumjeruhi vibaya mnadhimu wa chama hicho bungeni, mwakilishi wa jimbo la Lousiana Steve Scalise.
Mshambuliaji huyo aliekuwa na hasira dhidi ya rais Donald Trump na wabunge wa Republican, alipambana vikali na polisi kabla yeye mwenyewe kupigwa risasi na kufariki baadaye.
Watu wengine wanne walijeruhiwa katika shambulizi hilo.Rais Trump amemtembelea mbunge huyo katika hospitali mjini Washington alikofanyiwa upasuaji na kusema kwenye ukurasa wake wa twita kuwa yuko katika hali ngumu na kuwataka Wamarekani wamuombee.
Hali yake imeelezwa kuwa mbaya sana.
