Mshauri mkuu wa Rais Donald Trump kuhusu janga la covid-19, Anthony Fauci ameonya dhidi ya kulegeza vikwazo vya janga la virusi vya corona mapema na kurejesha hali kuwa ya kawaida nchini humo.
Akizungumza mbele ya bunge la seneti, Fauci ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza amesema kuna uwezekano wa kuzuka kwa wimbi la pili la maambukizi ambalo halitoweza kudhibitika endapo maisha yatarudi kama kawaida kwa sasa.
Rais Trump anataka vikwazo vilegezwe kwa haraka nchini humo na shughuli zirudi kama kawaida kutokana na uchumi ulioanguka.
Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kimeripoti kuwa watu milioni moja nukta tatu wameambukizwa virusi hivyo Marekani huku zaidi ya 80,000 wakiwa wamefariki dunia.
