Mshauri wa maswala ya usalama Michael Flynn Kuhojiwa na aliyekua mkuu wa upelelezi kawaandikia barua maafisa na rafiki zake.

In Kimataifa
     Maseneta wanaochunguza uhusiano uliopo kati ya Rais Donald Trump na Urusi wamemwagiza aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama nchini Michael Flynn afike mbele yao kuhojiwa. Wanataka atoe stakabadhi alizo nazo. Bwana Flynn alikataa kufanya hivyo majuma mawili yaliyopita.
Alilazimishwa kujiuzulu mnamo Februari baada ya kusema uongo juu ya mawasiliano yake ya simu na balozi wa Urusi nchini humo.
Wakati huo huo;
Aliyekuwa mkuu wa idara ya upelelezi nchini Marekani, James Comey, aliyetimuliwa kazini Jumanne, amejibu hatua hiyo kwa kuwaandikia barua maafisa katika idara hiyo na rafiki zake. Alisema hatapoteza wakati wake juu ya hatua iliyochukuliwa au jinsi ilivyotekelezwa na akasema kuwa kwa muda mrefu ameamini kuwa Rais ana kila sababu ya kumtimua kazini mkurugenzi wa FBI kwa sababau moja au hata bila sababu yo yote.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu